Kwa wanafunzi na walezi: Maagizo kuhusu masomo ya mbali kwa ajili ya shule ya sekondari

Kontakta Site Page

Site Page

Kontakta Umeå kommun

Telefon: 090-16 10 00

Besöksadress: Skolgatan 31A, 901 84 Umeå
Öppettider: Måndag-fredag kl. 8.00-17.00

Siku ya Jumanne, Machi 17, manispaa ya Umeå iliamua kufuata pendekezo la serikali kwamba elimu ya sekondari na ya watu wazima ifanyike kwa kutumia masomo ya mbali. Hapa kuna taarifa ya jinsi hii itatekelezwa kwenye shule ya sekondari.

Lengo letu ni kuendelea na utendaji lakini kwa njia tofauti. Tunafahamu kwamba hii inazusha maswali mengi, lakini tutaendelea kuwapatia taarifa, haswa kupitia Lärum lakini pia kupitia tovuti ya shule.

Taarifa ijumaa Machi 20

Tunapenda kutoa shukrani nyingi kwa wanafunzi na walezi kwa kazi yote mliyofanya wiki iliyopita! Wiki ijayo, tutaendelea na kazi yetu kupitia masomo ya mbali kulingana na ratiba iliyopo. Ikiwa una maswali yoyote unakaribishwa kuwasiliana na mshauri au mwalimu husika.

Taarifa jumatano Machi 18

Masomo kulingana na ratiba
Masomo ya mbali na ya moja kwa moja kupitia mtandao yataendela kulingana na ratiba iliyopo kwa kadiri inavyowezekana. Ukiwa mwanafunzi, utapata habari unayohitaji kwa ajili ya kozi zako kutoka kwa mwalimu wako kupitia chumba cha kozi (kursrum) husika. Ikiwa hupati habari kuhusu kozi yako huko Lärum, wasiliana na mwalimu anayehusika kupitia barua pepe au kwa njia ambayo umezoea kuwasiliana na mwalimu wako.

Hudhurio
Kwa vyovyote vile, tunataka uendelee vizuri ukiwa mwanafunzi na kufaulo masomo yako kwa kadiri iwezekanavyo. Kwako wewe mwanafunzi ni muhimu sana kushiriki masomo yako na kuchukua jukumu lako.

Tunakuomba ukiwa mlezi pia kumsaidia kijana wako kukabiliana na mabadiliko haya ili kujifunza kuwe rahisi iwezekanavyo.

Chakula cha mchana shuleni
Wanafunzi wanaokaa Manispaa ya Umeå na kusoma kwenye shule za sekondari za Dragonskolan, Forslundagymnasiet, Maja Beskowgymnasiet au Midgårdsskolan wanaweza kuchukua chakula cha mchana kwenye shule za msingi na sekondari zilizoteuliwa.

Ili kupata habari zaidi na kuagiza chukula ingia: www.umea.se/hamtaskolmat Länk till annan webbplats.

Tunawaomba wanafunzi na walezi kuhakikisha kwamba mnapata habari na kusoma taarifa tunazoweka huko Lärum. Ikiwa una maswali yoyote kuhusu mabadiliko haya au maswali mengine, unakaribishwa kuwasiliana nasi!

Taarifa jumanne Machi 17

Kwa kuwa manispaa ya Umeå imeamua kufuata pendekezo la serikali kwamba elimu ya sekondari na ya watu wazima ifanyike kwa kutumia masomo ya mbali, sasa tunapanga kwa ajili ya jambo hilo pamoja na wafanyikazi wetu. Utendaji wetu utaendelea lakini kwa njia tofauti. Tunaelewa kuwa hii inazua maswali mengi kwa wanafunzi na walezi, lengo letu ni kuendelea kuwapasha habari kuhusu jinsi kazi inavyoendelea. Hii itafanywa hasa kupitia idhaa hii, yaani Lärum.

Ili kushiriki masomo ya mbali, sisi tunakuomba ukiwa mwanafunzi kuhakikisha kwamba unayo/unajua yafuatayo:

- Kompyuta ya shule inayofanya kazi.
- Uunganisho wa mtandao unaofanya kazi.
- Vifaa vyako nyumbani (waya ya kuchaji, vifaa vya shule)
- Unajua jinsi ya kuingia Google (kupitia barua-pepe yako ya edu) na Lärum.

Je! Nimwendee nani nikihitaji utegemezi na msaada na mambo ya kiteknolojia?

Kuna msaada wa simu kwa maswali ya kiteknolojia Jumatatu-Ijumaa 07.45-16.30 (saa 1:45-saa 10:30) kupitia nambari ya simu 090-16 64 10. Pia kuna fomu ya mawasiliano ambayo unaweza kutumia ikiwa unataka kutuma swali lako. Maswali yanajibiwa kwa zamu. Kiunganishi cha fomu ya mawasiliano

Skriv ut
Senast uppdaterad: 27 april 2020
Sidan publicerad av: Therése Swärd